Cellulite ama kwa jina lingine cottage cheese ni sehemu ya ngozi
nene ambayo hutokea kutokana na mafuta yanayojaa chini ya ngozi na hivyo
kusababisha kukata mzunguko wa damu (blood circulation) katika sehumu
hizo. Kwa kawaida wanawake wengi ndo huwa na cellulite ila hata wanaume
pia. Cellulite huonekana zaidi katika sehemu za mapaja, nyama za mikono,
maeneo ya tumboni na hata miguuni.
Cellulite husababisha mabonde bonde kwenye ngozi kutokana na mafuta yaliyojaa chini ya ngozi.
Ultrasonic
massage treatment– Hii massage treatment ni ya moto inayofanywa na
kimashine kinachopitishwa juu ya ngozi (mahali penye cellulite).
Treatment hii husadia kuchoma na kusaidia stimulation na circulation of
blood around the cottage cheese area (unahitaji about 10 treatment) ila
hata ukishafanya hizi treatment inabidi uendelee kuzifanya kila baada ya muda flani bila hivyo cellulite inarudia pale pale.
Ila Dr. Oz wa Dr. Oz Show anashauri kufanya mazoezi na kuwa na diet
safi (kuacha kula vitu vyenye mafuta sana badala yake kula matunda
zaidi na kunywa maji kwa wingi). Anasema kwamba massages na liposuction
haisaaidii, kwasababu sana sana, kitu massage inachofanya ni kusugua ile
sehemu yenye mafuta (cellulite) na kuyarudisha chini kwa muda halafu
baada ya wiki ngozi inajirudia na kustreach na mimafuta (cellulite)
inarudia pale pale. Liposuction pia ndo hivyo hivyo, ni procedure inayo
fyonza mafuta kupitia machine lakini watu wanachosahau ni kwamba mafuta
haya yanapofyonzwa lile eneo lilobaki linatepeta/tupu (chukulia mfano wa
tobo lililojazwa mafuta ukiyatoa mafuta sio kwamba tobo ndo litajiziba,
litabaki pale pale na mafuta mengine yatakuja tena kujirundika). Hivyo
ndo maana hata ukiamua kwenda chini ya kisu ama machine kuyafyonza ama
kukata haya mafuta sana sana ni kujiongezea tuu kazi na gharama in the
long run.
Hivyo
basi, madocta hawa wanashauri kwamba kitu kikuu ni kufanya mazoezi
haswa kama kukimbia na kutembea haraka haraka., pia elipticals, na
muscle toning. Hizi ndo njia pekee zilizoonyesha kusaidia kuondoa
cellulite kabisa.
Ama unaweza kutumia njia za kienyeji kama kawaida…(home remedy)
Mahitaji:
1 – Chumvi kijiko cha chakula
1 – Kikombe cha water
½ – Juice ya limao
½ – (pilipili nyekundu iliyosagwa) cayenne pepper
Changanya maji na chumvi. Then ongeza juice ya limao, then ongezea cayenne pepper.
Koroga mchanganyiko wako. Halafu paka kwenye maeneo uliyo na
cellulite. Acha mchanganyiko wako ukae kwa muda kwenye ngozi halafu osha
ama oga na maji safi. Endelea kufanya hivi kwa muda na kuendelea mpaka
uone matokeo mazuri ama uridhike mwenyewe.
















0 comments:
Post a Comment