Kuliko kutumia kemikali katika kujipata shepu nzuri ni bora ukafanya
mazoezi ambayo baadae ya kutakupatia shepu nzuri unayoiitaji. Kuna mazoezi mbalimbali yanayokuza na kuyapa makalio na nyonga muonekano mzuri, zoezi mojawapo ni ’’squarts’’
yaani kuchuchumaa kwa kiswahili rahisi. Kufanya squarts, waweza tumia
uzito au waweza fanya squarts bila kutumia uzito wowote. Unachukua uzito
unaoweza kuhimili, na kuuweka mabegani (kumbuka uzito huu unatakiwa uwe
umewekwa pande zote kwa uwiano sawa ukiunganishwa na bomba ambalo ndiyo
unaliweka mabegani). Simama wima miguu yako ikiwa imetengana kiasi,
halafu chuchumaa taratibu, na kunyanyuka taratibu. Rudia mzunguko huu
mara 6 mpaka 8, kwa kila seti, na ni vema kufanya seti tatu mpaka tano.
Kumbuka waweza fanya squarts bila kuwa na uzito wowote, cha muhimu ni
kuikutanisha mikono yako pamoja nyuma ya kichwa wakati wote unapokuwa
unachuchumaa na kusimama. Ni muhimu kufahamu kwamba, kama unataka sehemu
zako za makalio kuongezeka ukubwa, basi ni vema kutumia uzito.
Thursday, October 23, 2014
Mazoezi kwa ajili ya kupata hipsi
1:32 AM
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)








0 comments:
Post a Comment