Skwati (squats) ni moja ya mazoezi mepesi na muhimu kwa mwili wa binadamu. Aina hii ya mazoezi ni nafuu na salama yasiyo na gharama yoyote na yanayoweza kufanywa nyumbani na bila mahitaji ya vifaa vya ziada.
Kwa ufupi
Skwati huufanya mwili kuwa mwepesi katika ufanyaji shughuli wa kawaida katika maisha kama kutembea, kucheza muziki, kupanda milima na nyingine nyingi zinazoushughulisha mwili na misuli.
Skwati ni mazoezi yanayofanywa zaidi na vijana wa kisasa
ili kutengeneza maumbo mazuri. Katika siku za karibuni wanawake nao
wameanza kuyajenga maumbile kwa mazoezi hayo.
Skwati ni aina ya mazoezi ya mwili yanayosaidia
kujenga na kuimarisha misuli. Aina hii ya mazoezi husaidia kujenga
misuli ya miguu, mikono ya mwili mzima na tumbo.
Aina hii ya mazoezi ikifanywa kwa ustadi na
umakini, inasaidia kujenga nguvu za mwili sehemu ya chini ya mwili na ya
juu ambayo kitaalamu inaelezwa kuwa ni muhimu kwa ajili ya ukuaji wa
misuli.
Mazoezi haya yanaelezwa kusaidia kuboresha ukubwa
wa misuli pale unapofanya mazoezi mengine ya mwili tofauti yakiwamo yale
yanayofanywa na vifaa maalumu vya mazoezi (gym).
Skwati huufanya mwili kuwa mwepesi katika ufanyaji
shughuli wa kawaida katika maisha kama kutembea, kucheza muziki,
kupanda milima na nyingine nyingi zinazoushughulisha mwili na misuli.
Mtu anayefanya mazoezi ya Skwati anakuwa na nafasi
nzuri ya kujenga na kuimarisha misuli sambamba na kuiweka misuli
katika nafasi nzuri ya kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.
Inaondoa mafuta
Njia moja bora na ambayo inaleta matokeo ya haraka
katika kupunguza kalori na kuchomwa kwa mafuta katika mwili ni
kuimarisha misuli.
Wataalamu wa masuala ya afya na mazoezi wanasema
katika kila msuli unaojengwa na kuimarishwa katika mwili, mwili hupoteza
kalori 50-70 kwa siku.
Hii ina maana kuwa kama unao uwezo wa kupunguza
kiasi kikubwa cha kalori kwa siku unakuwa na uwezo vilevile wa kupunguza
kiasi kikubwa cha mafuta katika mwili.
Kuimarisha viungo vya Mwili
Skwati vilvile huimarisha misuli ya miguu. Mtu
anayefanya aina hii ya mazoezi huweza kuwa na miguu imara yenye uwezo wa
kutembea bila usumbufu wala kupatwa na maumivu kama ilivyo kwa watu
wasio na mazoezi.
Hali hii humwezesha mtu anayefanya mazoezi haya kuwa na misuli
imara inayosaidia kuleta uwiano wa uzito wa mwili na kumwezesha mhusika
kuondokana na uwezekano wa kupata madhara katika mifupa.
Inazuia majeraha
Mara nyingi watu wanaovunjika viungo, kushtuka
miguu au mikono ni kwa sababu wana udhaifu katika misuli na tishu zilizo
katika viungo (joints).
Ufanisi katika michezo
Aina hii ya mazoezi hupendwa hupendelewa zaidi na
wanamichezo hasa wale wanaoshiriki katika mbio pamoja na kuruka viunzi.
Hii ni kutokana na umuhimu wake katika kuimarisha misuli na kuboresha
uwezo kwa wanamichezo.
Fanya mazoezi haya kwa vipindi hadi dakika 30 kwa
siku, mara tatu kwa kwa wiki kwani ni njia ya haraka ya kuchoma mafuta
mwilini.
Mafunzo ni njia ya haraka sana kwa kuchoma mafuta wa moyo na mishipa.








0 comments:
Post a Comment