Matunda

Badala ya kutafuna Sambusa, Popcorn na cookies au chocolate kila wakati bora muda wako uelekeze kwenye matunda, kama huwezi kupitisha lisaa bila kuweka kitu mdomoni.

Kunywa maji kwa wingi.

Maji ni kinywaji asilia na muhimu sana kwa afya yako, usipende kunywa sana soda au vinywaji vyenye sukari nyingi. Wengi wetu hupendelea kunywa zaidi chai au soda (vinywaji baridi kama Cocacola, Pepsi, Redull nk). Vinwaji vingi jamii ya soda vina gesi ambayo sio nzuri kwa afya yako kwasababu huongeza uwezekano wa mtu kupata vidonda vya tumbo..

Fanya mazoezi ya mwili na viungo.

Unapofanya mazoezi ya viungo unaongeza hewa ya oksijeni kwa wingi katika mapafu yako na wakati huohuo mwili nao unaunguza mafuta ili kutoa nguvu kwa mwili.

ASALI NA LIMAO

Asali na limao vinasaidia kupunguza mwili/uzitoUzito mkubwa wa mwili hupelekea kupata magonjwa mbali mbali kama ya moyo, kisukari, high blood pressure, arthritis,ini n.k.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Monday, November 3, 2014

Cellulite unayo ama hauna? Jinsi ya kuondoa Cellulite

 
Cellulite ama kwa jina lingine cottage cheese ni sehemu ya ngozi nene ambayo hutokea kutokana na mafuta yanayojaa chini ya ngozi na hivyo kusababisha kukata mzunguko wa damu (blood circulation) katika sehumu hizo. Kwa kawaida wanawake wengi ndo huwa na cellulite ila hata wanaume pia. Cellulite huonekana zaidi katika sehemu za mapaja, nyama za mikono, maeneo ya tumboni na hata miguuni. 
Cellulite husababisha mabonde bonde kwenye ngozi kutokana na mafuta yaliyojaa chini ya ngozi.
Ultrasonic massage treatment– Hii massage treatment ni ya moto inayofanywa na kimashine kinachopitishwa juu ya ngozi (mahali penye cellulite). Treatment hii husadia kuchoma na kusaidia stimulation na circulation of blood around the cottage cheese area (unahitaji about 10 treatment) ila hata ukishafanya hizi treatment inabidi uendelee kuzifanya  kila baada ya muda flani bila hivyo cellulite inarudia pale pale.
  
 

Mafuta yaliyojaa chini ya ngozi yanayosababisha mabonde mabonde kwenye ngozi






Ila Dr. Oz wa Dr. Oz Show anashauri kufanya mazoezi na kuwa na diet safi (kuacha kula vitu vyenye mafuta sana badala yake kula matunda zaidi na kunywa maji kwa wingi). Anasema kwamba massages na liposuction haisaaidii, kwasababu sana sana, kitu massage inachofanya ni kusugua ile sehemu yenye mafuta (cellulite) na kuyarudisha chini kwa muda halafu baada ya wiki ngozi inajirudia na kustreach na mimafuta (cellulite) inarudia pale pale. Liposuction pia ndo hivyo hivyo, ni procedure inayo fyonza mafuta kupitia machine lakini watu wanachosahau ni kwamba mafuta haya yanapofyonzwa lile eneo lilobaki linatepeta/tupu (chukulia mfano wa tobo lililojazwa mafuta ukiyatoa mafuta sio kwamba tobo ndo litajiziba, litabaki pale pale na mafuta mengine yatakuja tena kujirundika). Hivyo ndo maana hata ukiamua kwenda chini ya kisu ama machine kuyafyonza ama kukata haya mafuta sana sana ni kujiongezea tuu kazi na gharama in the long run. 
Hivyo basi, madocta hawa wanashauri kwamba kitu kikuu ni kufanya mazoezi haswa kama kukimbia na kutembea haraka haraka., pia elipticals, na muscle toning. Hizi ndo njia pekee zilizoonyesha kusaidia kuondoa cellulite kabisa.  
 




Ama unaweza kutumia njia za kienyeji kama kawaida…(home remedy)
Mahitaji:
1 – Chumvi kijiko cha chakula
1 – Kikombe cha water
½ – Juice ya limao
½ – (pilipili nyekundu iliyosagwa) cayenne pepper
Changanya maji na chumvi. Then ongeza juice ya limao, then ongezea cayenne pepper.
Koroga mchanganyiko wako. Halafu paka kwenye maeneo uliyo na cellulite. Acha mchanganyiko wako ukae kwa muda kwenye ngozi halafu osha ama oga na maji safi. Endelea kufanya hivi kwa muda na kuendelea mpaka uone matokeo mazuri ama uridhike mwenyewe. 


Mazoezi Ya Kujenga Misuli Ya Mwili Bila Kunyanyua Vyuma.

Tofauti na unyayuaji vyuma vizito, zipo njia nyingine za kukuza misuli na kufanya mwili kuwa katika hali ya mvuto kuliko hata ya myanyua vyuma, na kuufanya mwili kujijenga kwa usawa bila kuwa na utofauti wa ukubwa wa misuli ambao wanyanyua vyuma vizito wengi wao walivyo, haya hapa ni mazoezi kumi na matano yatakayokuweka vizuri kiafya na kimuonekano...
 
Push up
  Ni zoezi linalopanua kifua, kujenga kifua, kukuza misuli ya mikono ya ndani na nje na ni zoezi zuri la kuanzia, kama unataka kuwa na mwili wa kujijenga vizuri anza na hili zoezi.
 Pull ups

 Pull ups inafanyisha kazi kila misuli mwilini, hasa misuli ya mikono na mgongo, ukitaka uwe na nundu za mikono kama za Jean Claud Vandame hili ndo hasa zoezi lako.
 Plank

Ukishikilia hili zoezi bila kutingishika kwa dakika kadhaa, wewe kweli utakua una nia na kuubadilisha mwili wako liwe hekalu la mvuto. Zoezi hili linahitaji mabega yaliyoshiba na linafanyisha kazi misuli ya mikono, kiuno, mgongo, shingo na miguu na zoezi hili lina zawadi moja, linafanya tumbo lako likatike mara sita.
Roll Out
 

Hili zoezi linafanana na la nusu push up(Plank), ila linachobadilisha ni kusukuma nondo kuelekea mbele na kurudi, na jinsi unavyoendelea kusukuma nondo ndo ambavyo zoezi linavyozidi kuwa gumu, kwa hio unahitaji nia na kujitoa kweli, faida zake linajenga misuli ya mgongo, kiuno, kifua na kutanua mabega.
 Glute bridge
Zoezi hili linajenga mgongo na misuli yote inaouzunguka, ukiwa mkufunzi wa hili zoezi kinachofuata ni kuombwa namba tu na wasichana.   
 Iverted Row
Hili zoezi ni la mgongo, fuata kama picha inavyolionyesha, faida zake linafanya kifua kiwe kipana zaidi na mikono iwe na stamina zaidi. 
  
 Close Hands Push ups
Hili zoezi ni kwa ajili ya mikono, na ni kwa ajili ya nundu za ndani na nje ya mikono, na misuli yako inakua inakua kwa pamoja bila kutegeana, fanya hili zoezi na utaona mabadiliko makubwa kwenye mikono yako.  
 Star Plack
 Hili zoezi kidogo ni zito kidogo, na zoezi hili linalenga kifua na mabega pamoja na misuli ya miguu na mikono, na ni zuri kwa kukata tumbo. 
 Burpee
 Zoezi la kupunguza mafuta mwilini, zoezi hili linafanya mwili mzima uchemke kwa pamoja, ukiwa unafanya hili, unakua unafanyisha kazi kila kiungo cha mwili na kuondoa sehemu dhaifu mwilini. 
 Dip
 Zoezi la misuli ya nyuma ya mkono na linasaidia pia kwenye misui ya kifua na upanuaji wa mabega na kufanya kifua kikae vizuri, zoezi hili linahitaji nia na nguvu ili lifanyike kwa mpangilio unaotakiwa na linamzidi yule aliyelala kwenye benchi akinyanyua vyuma vizito. 
Bulgaria Split Squart
  Kichura chura cha mguu mmoja nyuma, kinafanyisha kazi misuli ya mapajani na kukufanya uwe na stamina zaidi, ukifanya hili kwa wiki kadhaa, kama kichura chura cha kawaida kilikua kinakupiga chenga basi utakua unafanya mara mbili ya zaidi ulivyokua unafanya. 
Suspended Push ups
  Push ups ni nzuri, ila ukiiongezea ugumu kidogo kwa kuiongezea suspenda, ni njia mojawapo ya kuiongezea misuli uzito, na kufanya iwe misuli yenye ujazo na ya muda mrefu tofauti na yule anaebeba vyuma vizito. 
Prone Back Extension
  Hili zoezi linahimalisha kiuno, tumbo na mgongo kwa ujumla. 
Pike Push ups
  Ukiwa mkongwe wa push ups, hili ndilo zoezi la mwisho la push ups na linasaidia kuimalisha mabega na kuongeza ubora wa viazi vyako vya mikono. 
Swiss Ball Ro-------+++++++llout
 Zoezi linavyozidi kuwa gumu ndo misuli inavyozidi kuongezeka, ukiweza kuzingatia haya mazoezi utajishangaa baada ya wiki tatu mfululizo ukiwa unayafanya.