Mtu anaweza kupungua kilo ngapi kwa wiki ni swali ambalo watu wengi
hujiuliza.Hasa pale wanapotaka kuanza arakati za kupunguza
uzito.Ni wazi kwamba watu wengi hupenda kufanya Dayati za muda mfupi na wapate matokea makubwa ya haraka.
Kiasi cha uzito unaoweza kupunguza kwa wiki hutofautiana kati ya mtu
na mtu.Ingawa nia na juhudi binafsi huchukua nafasi kubwa katika
hili,Kuna mambo engine yanayoleta tofauti hizo
1.Jinsi
2.Umri
3.Ukubwa wa mwili
4.Vyakula unavyokula
5.Mazoezi unayofanya
Nguvu joto za chakula (calories)
Nguvu za chakula yaani kalori(kwa kiswahilli), calories (kwa
kiingereza) ni kiasi cha nguvu ambacho hupatikana au hutolewa na chakula
kifikapo mwilini.vyakula vyote (vyote viendavyo kinywani) vinaidadi
fulani ya calories isipokua maji tu ambayo hayana calories.
Calories hufanya kazi mwilini kama ambavyo mafuta (petroli au dizeli) hufanya kazi kwenye
gari.Ili
gari iweze kutembea lazima mafuta yaungue ili kutoa nguvu ambayo
hutumika kutembeza gari,na jinsi unavyozidi kutembea ndivyo ambavyo
mafuta huzidi kuungua adi yanaisha
Mwili wa binadam nao hufanya vivyo hivyo,nguvu unazopata kwenye
chakula yaani calories,huungua ili kutoa nguvu ambayo inauwezesha mwili
wako kufanya mambo mbalimbali kuanzia kupumua,kutembea,kukimbia,na yote
ambayo mwiili
hufanya.Kadri unavyofanya shuguli nyingi zitumiazo nguvu ndivyo ambavyo calories hupungua mwilini.
Nusu kilo( 1/2 kg) ni sawa na calories 3500.Ili upunguze nusu kilo
katika uzito wako nilazima utoe calories 3500 katika mwili wako.Unaweza
kutoa calories hizo katika mwili wako kwa kupunguza kiasi cha calories
unazokula kwa siku au kwakuongeza mazoezi au kufanya kazi zinazofanya
utumie nguvu nyingi ili utumie nguvu za ziada ambazo mwili wako umetunza
(unene wako)
Makala yakitafiti iliyoandikwa na NBC NEWS mwaka 2009 ilisema kwamba
,kupunguza calories (chakula) ni muhim zaidi kuliko kufanya mazoezi
hasa kwa mtu mwenyenia ya kupunguza
uzito.Pia
ilisema mtu hupunguza uzito kwa haraka zadi endapo atapunguza kiasi cha
calories anazokula na kufanya mazoezi ya mwili ili kuunguza calories
ambazo mwili wake umetunza.
Utofauti
Jins ya mtu huchangia katika kuamua ni kiasi gani cha uzito anaweza
kupunguza kwa wiki..Kwa kawaida wanaume wanamisuli mingi kuliko
wanawake.Tafiti za Mayo clinic ya marekani zinaonyesha kwamba misuli
hutumia calories nyingi hivyo uwepo wake katika mwili hufanya mtu aweze
kupunguza uzito kwa
haraka.Hii hufanya wanaume waweze kupunguza mwili kwa haraka kuliko wanawake.
Pia tafiti hizo huonyesha kwamba mtu mwenye uzito mkubwa anauwezo wa
kupunguza uzito kwa hararaka kuliko mtu mwemye uzito mdogo,hasa
mwanzoni anapoanza kupungua.
Mazoezi.
Kiasi cha calories unazoweza kutoa mwilini unapofanya zoezi au shughuli nyingine hutokana na uzito wa
mtu.Mtu mwenye uzito mdogo hutoa calories chache na mwenye uzito mkubwa hutoa calories nyingi kw akiasi kile kile cha mazoezi.
Mfano:mtu mwenye kilo 72.5 atatoa calories 986 kwa kukimbia kwa
dakika 60,lakini mwenye kilo 108 atatoa calories 1,472 kwa kukimbia
dakika hizo hizo 60
Kadri unavyotoa calories nyingi mwilini ndivyo uzito unavyozidi kupungua
Dayati kali
Dayati kali hulenga kumfanya mtu apunguze uzito mwingi ndani ya muda
mfupi.Tafiti huonyesha kwamba asilimia kubwa ya uzito unaopotea
unapofanya dayati kali ni uzito wa maji mwilini.
Ni ngumu sana kwa mwili kutoa kilo 1 ya mafuta mwilini kwa
wiki.Hata
ivyo endapo utaendelea na dayati kali kwa muda mrefu basi unaweza
kupunguza mafuta ya mwili na hivyo kupunguza mwili kwa haraka.
Ukifanya dayati kali sana,ambayo inakufanya uingize calories chache
sana mwilini basi kunauwezekano wa kupunguza kilo ndani ya muda mfupi.
Magonjwa na matibabu
Historia ya afya yako ni Sababu nyingine inayochangia katika kujua
kiasi cha kilo unachoweza kupunguza kwa wiki.Magojwa yasababishwayo na
homoni za mwili hufanya iwe ngumu sana kupunguza uzito wa mwili.
Tafiti zinaonyesha kwamba baadhi ya madawa kama madawa ya kisukari na
dawa za uzazi wa mpango hufanya iwe ngumu kupunguza uzito.Baadhi ya
madawa pia hufanya mtu ashindwe kabisa kupunguza uzito na madawa mengine
hunenepesha mwili.
Ushauri
Endapo umekua ukifanya mazoezi na dayati kwa muda mrefu na hupungui
uzito,ni vyema ukamuaona Daktari wako na kumuelezea hali hiyo ili aweze
kutafuta chanzo cha tatizo hilo na kulitafutia ufumbuzi.
Kama unafanya juhudi za kupunguza uzito basi punguza kiasi cha
calories unazokula kwa siku na pia fanya mazoezi ili kuunguza calories
za akiba mwilini.
Hitimisho.
Naamini umeelewa nikwanini hakuna kipimo maalum cha kiasi cha uzito
ambao mtu anaweza kupunguza kwa wiki,kwani vigezo vyote hivi huchangia
katika kupungua.
Hata ivyo vitu kama msongo wa mawazo na kutokupata usingizi
wakutosha,pia huweza kuchangia mtu kupungua uzito au laa kuongeza uzito.
UNAWEZA KUPUNGUZA UZITO UKIAMU,HAIJALISHI UNAUZITO MKUBWA KIASI GANI
Vyanzo vya taarifa za makala hii.